Mwanasheria wa Yanga Sc, Patrick Saimon ameweka wazi kuwa mpaka sasa Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc na walimsainisha mkabata wa miaka mitatu na kumtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 - 2025.
“Yanga imeshutumiwa sana kuhusiana na sakata la Yusuph Kagoma, leo kama Yanga tumeamua tuongee kuhusu nafasi ya Yanga Kwenye sakata la Kagoma.
“Ilikuwa Machi 04, 2024 Yanga Sc ilianzisha mchakato rasmi wa maongezi ya kumnunua Kagoma, baada ya maongezi Singida Fountain Gate walifikia muafaka ulitoa kiwango na tukafikia makubaliano ya kulipa milioni 30 ya kumnunua Kagoma.