YANGA WANAONGOZA KWA MAMILIONI GOLI LA MAMA
WAPINZANI wa Yanga kimataifa, CBE SA ya Ethiopia wameipa Yanga jumla ya milioni 35 kwa kufungwa jumla ya mabao 7-0 ndani ya dakika 180 katika anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rekodi imeandikwa Septemba 21 2024 Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 6-0 CBE SA katika mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 35, Clement Mzize dakika ya 46, Aziz Ki dakika ya 74, 90, Mudathir Yahya dakika ya 88 na Duke Abuya dakika ya 90.
Yanga inatinga hatua ya makundi Ligi ga Mabingwa Afrika mara mbili mfululizo baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza msimu wa 2023/24.
Ushindi huo umewapa Yanga kiasi cha milioni 30 za goli la mama ilikuwa baada ya dakika 90 kugota mwisho. Hivyo CBE SA wameipa Yanga milioni 35.
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa ni jambo kubwa ambalo limefanywa na wachezaji na ushindu ni mkubwa kupatikana wakitinga hatua ya makundi.
Hadi sasa Yanga wamefanikiwa kuvuna kiasi cha Tsh Milioni 85, kwa bao la mama ambayo imetokana na mechi 4 za Ligi ya Mabingwa wakianza a Vital’O na CBE.
“Ni furaha kwetu na tunamshukuru Mama kwa zawadi. Furaha yetu kuona tumetinga hatua ya makundi haikuwa rahisi lakini wachezaji wamepambana.”