REFA SIMBA NA AL AHLI TRIPOLI HUYU HAPA
Refa asiye na uzoefu mkubwa wa kuchezesha mechi za kimataifa, Abdoulaye Manet (34) kutoka Guinea ndiye amepangwa kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simbana Al Ahli Tripoli itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili ijayo kuanzia Saa 10;00 Jioni.
Manet alipata beji ya urefa ya Fifa mwaka 2020 alianza kupangiwa mechi za kimataifa, Februari 21, 2021 ambapo alikuwa refa wa akiba wa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo Jaraaf ya Senegal ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Platinum ya Zimbabwe,
Mchezo wa kwanza kwa Manet kuchezesha ulikuwa ni wiki iliyopita, Septemba10 wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 baina ya Zimbabuwe na Cameroon ulioisha kwa suluhu,
Refa huyo amechezesha idadi ya mechỉ saba tu, ambapo sita alikuwa refa wa akiba na moja tu ndio alipuliza kipyenga
Hakuwahi kuchezesha mechi yoyote ya klabu Afrika akiwa refa wa kati, hivyomchezo huo wa Simba na Al AhIi Tripoli utakuwa wa kwanza kwake,