Oscar Oscar Amchana Mzize :Mchezaji wa Kawaida Sana Hajawai Ibabe Timu

 

Oscar Oscar Amchana Mzize :Mchezaji wa Kawaida Sana Hajawai Ibabe Timu

KUHUSU ubora wa mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Clement Mzize umekuwa na dosari kwa upande wa mchambuzi wa michezo Oscar Oscar ambaye alisema kwamba, mchezaji huyo licha ya kufunga mabao lakini hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu.

“Huu ni msimu wa tatu tunamshuhudia Mzize. Ni mchezaji mzuri sana, lakini hajawahi kufunga hata mabao 10 ya ligi. Hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu kwenye mazingira magumu na hana mabao mengi yanayokumbukwa na wengi.

“Natamani tungeacha mchezo wa kuongeza sifuri. Natamani tungeacha mchezo wa Waingereza. Mzize bado ni mchezaji ambaye kwenye nafasi tano anaweza kufunga bao moja. Bado anakua.”

“Kuna watu wameanza kumpa jina na la Didier Drogba. Ni vizuri mtu kuwa na ndoto kubwa, lakini ni vizuri zaidi kuwa na ndoto zenye uhalisia. Tuna kijana anaitwa Kelvin John. Ni Mtanzania mwenzetu. Ni kijana wetu na anacheza Ligi Kuu Denmark. Wakati anaanza kuchipukia alipewa jina la Mbappe. Hadi leo hakuna mfanano wowote.” Oscar Oscar

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad