MRITHI WA MGUNDA SIMBA NOMA....

 

MRITHI WA MGUNDA SIMBA NOMA....

Uongozi wa klabu Simba umemtangaza rasmi Kocha Yussif Basigi kuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake, Simba Queens akichukuwa nafasi iliyoachwa na Juma Mgunda.


Meneja wa Simba Queens, Seleman Makanya amesema Basigi raia wa Ghana yupo nchini akiendelea kukisuka kikosi cha timu hiyo anatarajiwa kuanza kuonekana katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii.


Amesema kocha huyo amejiunga na timu akitokea Hasaacas Ladies ya nchini kwao Ghana, mwaka 2015alipata medali ya dhahabu akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya Ghana (Black Queens) kwenye michuano ya All African Games.


“Tumemtambulisha Basigi kuwa kocha wetu mkuu na ameashaanza kazi rasmi na anatarajiwa kuwepo kwenye benchi la ufundi la timu hiyo akisaidiana na Mussa Hassan Mgosi, kuelekea katika mchezo wetu wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii,” amesema Makanya.


Kuhusu beki wao Daniella Ngoyi kutoweka kambini, meneja huyo amesema mchezaji huyo hayupo kambini na ameondoka kwa ruhusa maalum kwenda kwao DR Congo kwenda kutatua changamoto za kifamilia tofauti na inavyozungumzwa.


“Daniella yupo kwao ameondoka kwa ruhusa maalum kwa sababu ana matatizo ya kifamilia na hajatoroka kama ilivyokuwa kwa Aisha Mnuka ambaye tunahesabu ni mtoro kazini,” amesema meneja huyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad