MBWANA SAMATTA KUMFUATA SIMON MSUVA SAUDIA

 

MBWANA SAMATTA KUMFUATA SIMON MSUVA SAUDIA
MBWANA SAMATTA KUMFUATA SIMON MSUVA SAUDIA

Nyota wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika timu ya PAOK ya Ugiriki, Mbwana Samatta ‘Popat’ inaelezwa anajiandaa kumfuata Simon Msuva anayecheza soka nchini Saudi Arabia baada ya klabu ya Al Kholood iliyopanda Ligi Daraja la Pili nchini humo kutuma maombi ya kumtaka nahodha huyo wa Taifa Stars kwa mkopo.


Kama dili hilo litakamilika huenda Samatta akakutana na pacha anayecheza naye Taifa Stars, Msuva anayeichezea Al Najma katika ligi hiyo.


Samatta amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya kikosi cha PAOK na mkataba alionao na Wagiriki hao unatarajiwa kutamatika Juni, mwakani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad