Kocha Gamondi Presha Imeshuka Baada ya Yao Kurejea Uwanjani...



Kocha Gamondi Presha Imeshuka Baada ya Yao Kurejea Uwanjani...

Wakati Klabu ya Young Africans inaendelea kujifua Dar es Salaam ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA ya Ethiopia utakaopigwa Jumamosi ijayo jijini Addis Ababa, huku beki wa kulia wa timu hiyo, Yao Kouassi akikoleza moto baada ya kurejea uwanjani kutoka majeruhi.


Beki huyo aliyekuwa ameumia mazoezini wakati wakijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ameshusha presha ya watu wa benchi la ufundi akiwamo Kocha Miguel Gamondi, baada ya kuanza mazoezi makali na wenzake.


Kwa sasa Mlinzi huyo wa kulia ameanza mazoezi makali chini ya kocha wa Viungo Taibi Lagrouni, ambaye ndiye anayesimamia mpango mzima wa kusimamia Utimamu wake.


Yanga itavaana na CBE baada ya kila moja kuvuka raundi ya kwanza ya michuano hiyo, vijana wa Gamondi wakiing’oa kwa kishindo Vital’O ya Burundi kwa ushindi wa mabao 10-0, huku Wahabeshi wakiitoa SC Villa ya Uganda kwa mabao 2-1.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad