FREDDY AUKUBALI MOTO WA ATEBA…AITABIRIA SIMBA FAINALI

 

FREDDY AUKUBALI MOTO WA ATEBA…AITABIRIA SIMBA FAINALI

Straika wa zamani wa Simba, Freddy Michael ambaye alikuwapo uwanjani akiishuhudia timu yake ya zamani ikimkanda Mwarabu mabao 3-1 na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kimataifa kwa jumla ya mara 6.

Freddy alisema licha ya ushindi, lakini amekoshwa na Ateba, huku akiitabiria kufika mbali.

“Nimekuja kuangalia mechi, nimekuja kuwaona rafiki zangu, unajua kwenye kikosi nina marafiki zangu wengi sana.

“Simba imecheza vizuri, imeshinda, ina wachezaji wazuri, imesajili wachezaji wengi wenye ubora, Ateba ni straika mzuri na amefunga, nadhani wataenda kufanya vizuri msimu huu, nawatabiria fainali,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad