Kuna burudani fulani huwa inatokea Kiungo wa Boli Kapteni Kucho Awesu Awesu akiwa na mpira mguuni.
Awesu Ali Awesu huwa analainisha sana mambo, simple tu mali inamtii ,anaweka moja njiani then anaitaka tena mbungi.
Huwa kila nyakati natamani aweze kupasiwa mpira ili nione burudani kupitia miguu yake.
Udambwi dambwi umejaa bwana.
Anafurahisha sana kumtazama,ukienda kichwa kichwa unapigwa kikoi mapema tu na Mali inakua bado kwenye umiliki wake.
Nafikiri kitu cha muhimu sana kwake nilichokiona kama changamoto ni PHYSICAL FITNESS (UTIMAMU WA KIMWILI) akiongeza hiyo fitness itamsaidia sana kwenye ile mipambano ya 1v1 na kuishinda tofauti na sasa ambapo naona kama kwenye matukio ya 1v1 anashindwa mengi.
Huyu captain Lucho (Awesu) ni fundi.