ALLY KAMWE AWAKARIBISHA FEI TOTO NA SILLAH KUCHEZA YANGA...


“Nimemsikia FeiToto akisema hana shida ya Eng Hersi Said .. wanaongea na anapokea pia ushauri mwingi kutoka kwenye Ubongo wa @caamil_88

“Feitoto pia kasema yuko tayari kucheza tena ndani ya Jezi bora aipendayo ya @yangasc.

“Nimemsikia yule winga Sillah akionyesha tamaa yake ya kutaka kuja Yanga binafsi haijanishtua sana.

“Hivi sasa ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi ya @yangasc ili afikie kilele cha ubora wake.

“Kauli za hao wachezaji wawili kutoka Chamazi, zimeonyesha ni kwa kiasi gani daraja la utu wa viongozi na ubora wa Kikosi cha @yangasc ulivyo hivi sasa.

“Niseme tu tajiri Gsm ameshasikia kilio cha Sillah na Wananchi Tumeshamsamehe Feitoto.

“Hawa ni wachezaji wazuri wanaostahili kucheza CAF CHAMPIONS LEAGUE kwenye Hatua kubwa kubwa na kufaidi bonus ya hela ya Rais wa Nchi.

“Nichukue fursa hii kumkaribisha Feitoto na Sillah waje New Amaan Complex kuungana na Wananchi tukiishangilia Timu yetu ya @yangasc.

“Tiketi za Ndege, gharama za Hotel, kula na kunywa ni juu yetu sisi .. wao jukumu Lao ni kutoroka tu kule Mbande na kuja kula raha Zanzibar

“Mwenzao Dube alianzaga kushangilia Jukwaani sasa tunamshangilia yeye”. Ameandika Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad