Ahmed Ally 'Yanga Mkimtaka Kagoma Subirini Miaka 10'

 

Ahmed Ally 'Yanga Mkimtaka Kagoma Subirini Miaka 10'

AFISA Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amewatania watani zao Yanga kama wanamtaka kiungo wao Yusuph Kagoma wasubiri misimu 10, ndiyo watamuacha akatafute changamoto mpya.


Hii ni kama ilivyokuwa kwa wachezaji wao waliopita Jonas Mkude, Clatous Chama ambao wamewaacha na wakaenda kujiunga na Yanga.


“Kwa mfano klabu yenu inampenda sana Yusuph Kagoma yaani kila mkilala mnamuota, roho zinawauma kumkosa na mnataka aje kwenu, Cha kufanya ni kuwa na subira”


“Kwa sasa Kagoma ana maika 23 na Isha Allah atakaa Simba kwa miaka 10+ akifikisha miaka 33 au 35 ndio atakuja kwenu”


“Yaani mfumo ni ule ule kama mlivyomsubiri Mzambia kwa miaka 7 au mlivyomsubiri namba 20 kwa miaka 15, Kagoma nae ni hivyo hivyoo ila kwa sasa ni Mali halali ya Simba”Ahmed Ally Afisa Habari wa Simba

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad