Unaambiwa Hivi Ndivyo AZIK K Alivyonogesha Kilele Cha Wiki ya Wananchi

Unaambiwa Hivi Ndivyo AZIK K Alivyonogesha Kilele Cha Wiki ya Wananchi

Unaambiwa Hivi Ndivyo AZIK K Alivyonogesha Kilele Cha Wiki ya Wananchi

MCHEZO wa kirafiki kati ya Yanga na Red Arrows ya Zambia, ulimalizika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam kwa wenyeji kushinda kwa mabao 2-1.

Timu hizo zimekutana katika mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’, ambapo Red Arrows ilitangulia kupata bao kupitia kwa, Ricky Banda dakika ya sita kisha Mudathir Yahya kuisawazishia Yanga dakika ya 64.

Bao la ushindi la Yanga lililoamsha mzuka kwa mashabiki wa timu hiyo limefungwa na Stephane Aziz Ki kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90, baada ya beki wa kikosi hicho, Nickson Kibabage kufanyiwa madhambi eneo la hatari.

Ushindi huo ni wa tatu kwa Yanga katika tamasha hilo tangu lilipoanza mwaka 2019, ambapo ilianza kwa kuichapa timu ya Aigle Noir ya Burundi mabao 2-0, mwaka 2020.

Katika mchezo huo, mabao ya Yanga yalifungwa na waliokuwa nyota wa kikosi hicho Mghana, Michael Sarpong na Tuisila Kisinda ‘TK Master’.

Ushindi mwingine wa kikosi hicho katika kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’, kilikuwa cha mwaka jana, ilipoifunga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini bao 1-0, lililofungwa na Mzambia, Kenney Musonda.

Yanga imeialika Red Arrows ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia, baada ya kushinda michezo 21, kati ya 34, sare minane na kupoteza mitano huku ikikusanya jumla ya pointi 71.

Mbali na hilo ila Red Arrows ni mabingwa wa Kombe la ABSA 2024, huko Zambia huku ikitwaa ubingwa wa Kagame mwaka huu jijini Dar Es Salaam, baada ya kuifunga APR ya Rwanda kwa mikwaju ya penalti 10-9, kufuatia timu hizo kufungana bao 1-1, ndani ya dakika 120.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.