Simba Bado Yakomaa na Saini ya Fei Toto

Simba Bado Yakomaa na Saini ya Fei Toto

 Simba Bado Yakomaa na Saini ya Fei Toto

Mchambuzi wa masuala ya Soka, Hans Rafael kutoka Crown Media amesema kuwa Klabu ya Simba ipo kwenye mipango ya kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto'.


Itakumbukwa kuwa, Fei Toto aliyekuwa akiitumikia Yanga aliomba kuvunja mkataba jambo lililoibua sekeseke lakini mwisho wa siku akaruhusiwa ndipo alipojiunga na Azam FC.


Msimu uliopita Fei Toto amefunga mabao 19 na assists 6 akiwa mchezaji pekee mzawa aliyehusiwa kwenye mabao mengi huku pia akifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho.


"Fei Toto ana mkataba na Azam hadi 2026, ndani ya huo mkataba kuna kipengele cha kuvunjwa endapo italipwa $500,000 (1,355,000,000).


"Azam wanataka kumuongezea mkataba mpya ila hadi sasa Fei hajakubali kusaini. Nachoweza kusema Fei anakaribia kurejea Kariakoo, Simba wana mpango wa ku-push hilo dili mwezi Januari," amesema Hans Rafael.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.