Saleh Jembe: Mashabiki wa SIMBA wana haki ya kumzomea Kibu

 

Saleh Jembe: Mashabiki wa SIMBA wana haki ya kumzomea Kibu

Mchambuzi mahiri wa soka, Saleh Ally Jembe amesema mashabiki wa Simba waliomzomea mchezaji wao, Kibu Denis kwenye mechi dhidi ya APR ya Rwanda kwenye Simba Day, walikuwa sahihi kutokana na utovu wa nidhamu waliofanyiwa na mchezaji huyo.


Saleh amesema Kibu Denis pia hakupaswa kucheza kwenye mechi hiyo kwani hakushiriki kwenye mazoezi ya pre-season kama wenzake kutokana na sakata lililokuwa likiendelea kati yake na uongozi wa Simba.


Mchambuzi huyo pia amesema taarifa alizonazo ni kwamba Simba haimhitaji tena aliyekuwa golikipa wake, Aishi Manula na ndiyo maana hata kwenye utambulisho wa wachezaji Simba Day jina lake halikuwepo lakini akatahadharisha kwamba busara zinapaswa kutumika kwani yapo mengi mazuri ambayo Manula ameyafanya akiwa Simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.