Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza tarehe rasmi za michezo ya miashindano ya Ngao ya Jamii kwa msimu wa 2024-25, ambapo michezo hiyo imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 8 hadi Agosti 11, 2024. Hii inaashiria kuanza kwa msimu mpya wa soka nchini, ukiwa unatarajiwa kua msimu wenye ushindani mkubwa na ubora wa mpira wa hali ya juu zaidi.
Ratiba ya Ngao ya Jamii 2024
Msimu mpya wa soka Tanzania unaanza kwa kishindo! Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza ratiba kamili ya michezo na viwanja vitakavyotumika katika michuano ya ngao ya jamii ya mwaka huu. Msimu wa 2024/2025 wa michuano ya Ngao ya jamii umepangwa kuanza Agosti 8 ambapo timu nne zitachuana vikali kumtafuta bingwa wa ngao wa jamii hadi Agosti 11, 2024.
Hii apa Ratiba Nusu Fainali Ngao ya Jamii 2024/2025
Tarehe Mechi Uwanja
8 Agosti 2024 Azam FC vs. Coastal Union Uwanja wa Amaan, Zanzibar
8 Agosti 2024 Young Africans vs. Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa, DSM
Ratiba ya Ngao ya Jamii 2024
Agosti 8 itakuwa siku ya kusisimua kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania. Wanaramba ramba Azam FC watavaana na Wagosi wa Kaya, Mangushi Coastal Union katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Wakati huo huo, Timu ya wananchi Young Africans watapambana na mahasimu wao wa jadi Simba SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Ni vita ya wakubwa!
Ratiba Fainali Ngao ya Jamii 2024/2025 & Mshindi wa Tatu
Tarehe Mechi Uwanja
11 Agosti 2024 Mshindi wa Tatu Uwanja wa Benjamin Mkapa, DSM
11 Agosti 2024 Fainali Uwanja wa Benjamin Mkapa, DSM
Baada ya michezo ya nusu fainali, timu zitakazopata ushindi zitatinga fainali. Mshindi wa tatu ataamuliwa tarehe 11 Agosti katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Na siku hiyo hiyo, fainali kuu itafanyika ambapo bingwa mpya wa Ngao ya Jamii atatawazwa.
Msimu uliopita, michezo ya Ngao ya Jamii ilifanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, na kuna matarajio kuwa viwanja vingine vya kisasa vitaweza kutumika kwa msimu huu. TFF inatarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu ratiba na viwanja kabla ya kuanza kwa michuano.
Michezo ya Ngao ya Jamii ni kipimo muhimu kwa timu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu. Timu zitakuwa zikitumia michuano hii kujaribu vikosi vyao na kupanga mbinu zitakazotumika katika msimu mzima. Mashabiki nao wanatarajia burudani ya hali ya juu kutoka kwa timu hizi kubwa nne