Msemaji wa Vital'O: Rais Samia na Sisi Tupatie Milioni 5 Kila bao

 

Msemaji wa Vital'O: Rais Samia na sisi tupatie milioni 5 kila bao

Msemaji wa timu ya Vital'O Fc, Arsene Bucuti amemuomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwapa Tsh milioni tano kama zawadi kwa kila bao iwapo watamfunga Yanga kwenye mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika.


Yanga Sc kwenye mchezo wao wa awali wa Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika waliifunga Vital'O mabao 4-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na sasa watarudiana tena tarehe 24 Agosti,2024.


“Namwambia Rais wa Yanga, Eng. Hersi, msemaji Ally Kamwe na Haji Manara, nimepewa suti moja ninarudi na suti tano. Kwenye ule mchezo, Vital’O tutawafunga bao 5-0 Yanga. Tunatoa ombi kwa Rais Samia Suluhu, iwapo na sisi tutafunga bao 1, na sisi atupatie sh milioni 5, tukifunga bao 5 na sisi atupatie sh milioni 25 zetu.


“Yanga ilivyotufunga bao 4 nikakumbuka Yesu alivyotundikwa msalabani, lakini nikaona Yesu alifufuka siku ya tatu, na sisi tutafufukia kwenye Uwanja wa Mkapa pale. Sisi mambo tumeshamaliza, mabao matano tu.


“Kama Mlandege inaipiga Yanga kwa nini Vital’O isimpige Yanga, leo nakwenda Unguja kwa wazee wangu kuwauliza ni jinsi gani huwa wanaweza kuwafunga Yanga na Simba na Azam,” amesema Baccuti

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.