Mchambuzi Adai Yanga Ipongezwe Kwa Kutoruhusu Mchezaji Mzize Kuuzwa

 

Mzize is Not For Sale, Niwapongeze Yanga Kwa Huu Msimamo, Tulinyanyaswa Sana

MZIZE IS NOT FOR SALE!

Wydad Casablanca wametuma ofa ya tatu kwenda Yanga yenye thamani ya $300,000 (tsh 814,500,000) pia kuna ongezeko la $50,000 kama Wydad watatwaa ubingwa wa Ligi kuu + $50,000 endapo Wydad watatwaa ubingwa wa Throne Cup + $50,000 endapo Mzize atafunga goli tano.

Kusema ukweli hiyo ofa ni kubwa ila Yanga wameipiga Chini…..siyo tu kupigwa chini ila hata Wydad hawakujibiwa.

Msimamo wa Yanga ni mmoja “Mzize hauzwi” (Mzize is not for sale).

Kwanza niwapongeze Yanga kwa huu msimamo maana siku za nyuma hiki kitu kilikuwa ni ndoto,wakubwa walizoea kuvidhoofisha vilabu vyetu,mchezaji yeyote akionyesha ubora mwisho wa msimu anabebwa na wakubwa.

This time Yanga wamechoka kuwa wanyonge,ni wazi wanataka kushindania ubingwa wa Africa.

Aziz Ki amebakishwa kwa $500,000 (tsh 1.3 bilion) halafu Bado wanaonyesha kiburi cha kumbakisha Mzize.

Guys mpira wetu unakua kila mwaka timu zetu zimeanza kuonyesha ukubwa…muda wa mateso umepitwa na wakati.

Mchambuzi Hans Rafael

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.