Kilichowaponza Azam FC kwa APR ni hiki, Dabo anaondoka?

 

Kilichowaponza Azam FC kwa APR ni hiki, Dabo anaondoka?

Waoka mikate Azam FC wameondolewa rasmi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa APR FC ya Rwanda.


Mchezo wa kwanza Azam FC walikuwa nyumbani na kufanikiwa kupata ushindi wa goli moja lakini mambo yamekuwa magumu kwao kwenye mchezo wa ugenini na kupoteza mchezo huo.


Magoli ya APR FC yamefungwa na Ruboneka dakika ya 45 na Mugisha dakika ya 62, na kufanya mchezo huo matokeo ya jumla 2-1.


MAMBO SITA KUTOKA AMAHORO STADIUM KIGALI RWANDA: APR DHIDI YA AZAM FC.


1.Nilikuwa bize sana kutazama mechi ya APR dhidi ya Azam Fc, Ilikuwa mechi bora sana kuitazama lakini matokeo Yameniumiza sana kama Mtanzania.


2.Kipindi cha kwanza sijui Kocha Dabo aliwaza nini kuingia kwa mtindo wa kupoteza zaidi Muda kitu ambacho hakikuwa kizuri kwao.


3.APR hawakuwa na shughuli nyingine, wao walikuwa wanakesha katika lango la Azam Fc, Wakipoteza mpira chap wanarudi kuusaka wakiupata wanashambulia lango la Azam fc kwa kasi kubwa sana.


4.Azam FC wakiwa wanaenda kushambulia, walikuwa wanaacha space kubwa mno, Rest defence ilikuwa na shape ya mtu Tatu Bangala, Mendoza na Bitegeko. Kitu ambacho kilikuwa kinawapa wakati mgumu kudeal na kauta attacks za APR Kulikuwa na 3v4 nyingi sana.


5.Amahoro iliitika na APR walijiaanda vilivyo kufanya burudani, kila mpira waliougusa kwao ilikuwa dhahabu, Hawakutengeneza nafasi nyingi lakini zile chache ambazo nazo zilikuwa nusu nafaso (Half chance) walizitumia vema sana.


6.Azam Fc utaendelea kuwadai mentality kuelekea mechi kubwa na zenye maamuzi kama hizi, wachezaji walikuwa kawaida utazani wako kwenye show za nbc. miili haikuonesha kiu ya ziada.


NB. Kwa hiyo Azam FC wamepata sh milioni 5 tu za Mama? Mmmh wakati wengine wamepata mishahara ya kulipana huko.


Azam FC bado Wana Imani Kubwa na Benchi lao la Ufundi Chini ya Mwalimu Yousouph Dabo.


Uongozi unaamini wapo Kwenye Mradi ambao ufanisi wake huwezi kuupima Kwa matokeo dhidi ya APR.


Azam baada ya kurejea leo alfajiri wanajiandaa kuwakibili JKT Tanzania Jumatano kwenye mchezo wa Ligi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.