Wakili Yanga: Wanaotaka Hersi aondoke, wanatumika

 

Wakili Yanga: Wanaotaka Hersi aondoke, wanatumika

Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick amesema Club imegundua Walalamikaji Juma Ally na Geofrey Mwaipopo waliofungua kesi wakitaka Rais wa Club hiyo Eng.Hersi Said na Viongozi wengine waachie ngazi, kuna Watu wapo nyuma yao na wanatumika kuleta vurugu ambapo kwa kushirikiana na Vyombo vya usalama, Yanga imeanza kufanya uchunguzi ili kuwabaini walio nyuma yao.


Akiongea leo July 17,2024 Jijini Dar es salaam, Simon amesema “June 06,2024 Club ilipata taarifa kwamba kuna kundi limepeleka maombi Mahakama kuomba wapewe Uongozi wao, Rais Eng. Hersi akaelekeza Timu ya Mawakili kufuatilia hii kesi, baada ya kupewa faili la Mahakama na kulipitia sisi kama Club tuligundua kesi iliendeshwa kwa upande mmoja kwa hawa Watu kugawana majukumu wengine wakae upande wa Mlalamikaji na wengine wa Mlalamikiwa”


“Pili tumegundua Juma Ally Abeid alighushi sahihi ya Club kwa kujifanya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Club, alighushi sahihi ya Mama Fatma Karume akidai Mwakilishi wa Mama Fatma huku Mama Fatma hajui kinachoendelea, pia alighushi sahihi ya Juma Katundu, tuligundua pia Juma Ally na Geofrey Mwaipopo sio Wanachama wa Club ya Yanga, hivyo hawakuwa na uhalali wa kisheria kusimama kujadili masuala yanayohusu masuala ya kikatiba ya Yanga”


“Club pia imegundua kuna Watu wanawatumia na wapo nyuma ya hawa Watu kuvuruga amani na tayari Club kushirikiana na Vyombo vya usalama tumeanza kuwafanyia uchunguzi walio nyuma ya hawa Watu na wakibainika wote watapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kama ni Wanachama na Mkutano Mkuu utachukua hatua”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad