Kwenye Kikosi cha Young Africans, tangu aondoke aliyekuwa mshambuliaji wao, Fiston Kalala Mayele wameshasajiliwa washambuliaji sita (6) ili kuziba pengo lake na bado wanasaka mbadala sahihi wa Mkongomani huyo.
Waliosajiliwa kuziba pengo la Mayele;
1- Hafiz Konkoni >> Hayupo
2- Joseph Guede >> Hayupo
3- Clement Mzize
4- Kennedy Musonda
5- Prince Dube
6- Jean Baleke.
Wachezaji sita hao dhidi ya Kalala mmoja, bado anasakwa mrithi wake na wawili tayari wameaga shindano, ni sahihi kusema wamefeli?
Viatu vya King Mayele vimekuwa vizito sana mpaka sasa kutoka kwenye eneo lake la asili (striker) tunasubiri kuona Prince Dube kama vitamtosha viatu hivyo, ijapo Clement Mzize anajitahidi sana kwa nafasi yake.