Mo Amtaka Feisal Toto Simba Kwa Udi na Uvumba


Mo Amtaka Feisal Toto Simba Kwa Udi na Uvumba

Klabu ya Simba imefungua mazungumzo na Azam Fc kwa ajili ya kumtaka kiungo mshambuliaji Feisal Salum 'Fei Toto', imefahamika

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba, imethibitisha kuwa tayari mabosi wa Simba na Azam Fc wamekutana mara mbili na kuna matumaini ya makubaliano kufikiwa

Simba ina makubaliano binafsi na Fei Toto kuhusu maslahi yake, kilichokuwa kimebaki ni makubaliano baina ya klabu juu ya ada ya uhamisho

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ameuwekea kipaumbele usajili wa Fei Toto kwani anaamini mchezaji huyo ataongeza ubora kwenye eneo la kiungo cha ushambuliaji hasa baada ya Clatous Chama kuondoka

Azam Fc wamekuwa 'wazito' kumuachia Fei Toto kwa kuwa nao watashiriki michuano ya Kimataifa (Ligi ya Mabingwa) msimu ujao lakini tajiri 'Mo' ameonyesha utayari wa kununua mkataba wa Fei ili kuhakikisha anatua Msimbazi

Fei Toto alimaliza msimu uliopita akiwa kinara wa mabao katika kikosi cha Azam Fc akifunga mabao 19 na kutoa assist 7

Msimu wake mmoja na Azam Fc umetosha kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi kwa mchezaji wa Azam Fc katika msimu mmoja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.