Muda Mfupi tu baada ya kupokea kipigo cha Magoli 4-0 kutoka kwa klabu ya Yanga , Tayari Kimenuka huko Afrika Kusini kwa mashabiki wa Kaizer Chief kuanza kumkataa kocha wao Mpya Nasraddine Nabi na Kumuona hafai.
Yanga ilitembeza dozi ya kikubwa kwa Amakhosi, Magoli yakifungwa na Prince Dube, Aziz Ki mabao 2, na Clement Walid Mzize.
Mchezaji wa zamani wa Kaizer Chief Junior Kanye ambaye kwa sasa ni Mchambuzi wa soka nchini humo, aliweza kutoa maoni yake huku akishangazwa na mashabiki wa timu hiyo kuwa na matarajio makubwa ya kuifunga Yanga yenye ubora mkubwa kwa sasa.
“ Mashabiki wa Kaizer Chiefs wanatakiwa kuelewa uhalisia kuwa Young Africans ni timu bora kwa sasa Afrika. Kaizer Chiefs bado inajitafuta, ” – Junior Kanye.
“ Nilijua kuanzia mwanzo wa shindano la Toyota cup kuwa Kaizer Chiefs watapoteza dhidi ya Yanga SC. Wachezaji wa Yanga wako na nguvu kiakili na wameweza kucheza katinga ngazi ya juu ya mashindano makubwa kama ya (CAF), Hivi karibuni wametoka kuifunga Simba (5-1), timu iliyo kwenye kumi bora (CAF), ” Alisema Junior Kanye
“ Kama Yanga wameweza kuifunga Simba (5-1) unategemea nini kwa Kaizer Chiefs, si ajabu kufungwa hizo goli (4-0). Yanga ni Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara .. Wakati mwingine mashabiki wananishangaza, wanakuwa na matarajio makubwa, yaani waliwaza kuwa Kaizer Chiefs itaifunga Yanga seriously?! timu bora kama Yanga, ”
“ Ukweli ni kwamba mashabiki wanatakiwa kujua uhalisia na kutotarajia mafanikio makubwa katika muda mfupi. Nabi na benchi lake la ufundi wanahitaji zaidi ya misimu (2) kuitengeneza Kaizer Chiefs bora, ”
Habari Mpya za Yanga