Eng Hersi wa Yanga |
Yanga Ruksa Kusajili, Walipa Madeni Yao Yote.....
Awali, mchezaji huyo raia wa Zambia alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kwa kushindwa kumlipa ujira wake. Kambole alishinda kesi hiyo, na Young Africans ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza uamuzi huo na kusababisha ifungiwe kusajili.
Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Young Africans kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.