Tetesi: Kipre Junior kutua Yanga, Carno kumfuata Inonga

 

Tetesi: Kipre Junior kutua Yanga, Carno kumfuata Inonga

Vita ya timu za Yanga na Azam kwenye ushawishi wa wachezaji imezidi kupamba moto ambapo baada ya sakata la Frank Domayo, Fei Toto, Salum Abubakar 'Sure Boy', Prince Dube sasa inaelezwa kuwa Wananchi wana mpango wa chinichini kusepa na Mkali wa Asisti msimu uliopita Kipre Junior.


MICHEZO UPDATES Joshua Mutale alikuwa MVP wa pili msimu uliopita. Mchezaji bora chipukizi wa msimu 2022. Mchezaji bora wa mwaka wa mashabiki 2023.


Amehusika mara 15 kwenye magoli ya msimu huu na kwa sasa anachukuliwa kuwa mchezaji bora wa Power Dynamos.


WAZAMBIA KUTUA SIMBA SC


Kama nilivyoripoti hapo awali Crescentius Magori kwa sasa yupo nchini Zambia kufawatilia usajili wa wachezaji 2 mmoja ni Joshua mutale na mwingine ni kiungo mshambuliaji (jina bado halijapatikana) ili waweze kusajiliwa na klabu hiyo msimu ujao.


Ndani ya wiki inayoanza simba sc itaanza kugawa THANK YOU ni ishara ya kuingiza vyuma vipya .


Kaa mkao wa kula kamati mpya ya usajili inakuja na usajili mpya.


CARNO BIEM KUMFATA INONGA WA SIMBA


Beki wa kati Carno Biem mwenye umri wa miaka 23, raia wa Kongo, amesaini mkataba wa msimu 1 na Al-Hamriyah FC ya Falme za Kiarabu.


Singida Fountain Fc imemaliza ligi kuu ya Tanzania na Beki huyo anachukuliwa kama beki Bora wa Kati kwenye kikosi hicho.


Nahodha huyo wa Singida alikuwa anatakiwa katika vilabu vingi mwanzoni mwa kipindi hiki cha usajili.


Katika ligi kuu ya NBC PREMIER LEAGUE real model wake alikuwa anasema ni HENOCK INONGA anamtazama kama real model wake.


Ahly vipi huko? Al Ahly Benghazi Wameinasa Saini ya Mshambuliaji wa Al Hilal Ondurma John Mano (22)


John Mano amesaini mkataba Wa miaka miwili kuwatumikia miamba hiyo ya Libya ????????.


Yanga imeanza mazungumzo na Singida Black Stars kwa ajili ya kumpata kipa wa timu hiyo, Khomeiny Aboubakar. Khomeiny amekuwa na msimu mzuri na kikosi hicho, anatajwa kama mbadala wa Metacha Mnata anayeondoka baada ya kuhudumu kwa miezi sita ya mkopo na Yanga inamtaka iwapo itamkosa Yona Amos wa Tanzania Prisons.


Deal Done; Winger, Victorien Adebayor atawasili Nchini Tanzania ???????? mwezi huu kukamilisha usajili katika klabu ya Singida Black Stars (Ihefu).


Adebayor msimu huu katika ligi kuu ya Niger akiwa na klabu ya Jongorzo :


◉ 14 - Games. ◉ 22 - Goals scored.


Adebayor aliachwa na klabu ya RS Berkane ???????? akarejea nyumbani kujitafuta. Amejipata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.