Mo Dewji Tajiri Mpweke zaidi Kwenye Historia ya Mpira wa MiguuUkimtazama MO Dewji basi naamini unamtazama Tajiri Mpweke zaidi kwenye historia ya mpira wa miguu, ni simulizi ya Kijana kutoka Singida ambayo ndani imejaa usaliti, maslahi na tabasamu linaloficha maumivu mengi, shuka sambamba na mimi.

Baada ya upepo mkali sana wa vuguvugu la mabadiliko ndani ya Simba, kwa taarifa zangu za kiuchunguzi MO hakutaka kurejea Simba kama Mwenyekiti wa Bodi bali alimpigia Rafiki yake mmoja wa karibu sana ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la Umma aende kuvaa viatu vyake kama Mwenyekiti.

Swahiba wake alikataa kabisa na kumwambia Mtu pekee anayehitajika na anaweza kuikoa Simba kwasasa ni yeye MO mwenyewe hivyo arejee kusimamia ile ndoto ambayo mbegu imegoma kuchipua Jangwani, mvua hakuna na jua limegoma kuzama ili tuione siku mpya.

Kwanini MO Dewji ni Tajiri Mpweke zaidi? Nitakupa kisa kimoja kuhusu Mtu wa kuitwa JOSE ANGEL SANCHEZ MERIN hii ni mashine nyuma ya Florentino Perez wa Real Madrid, aliyehudumu vipindi vitatu tofauti ndani ya Real Madrid kwa Marais wawili tofauti yani Perez na Ramon Calderon, huyu anahusikaje?

Ndio! MO anamkosa Jose Angel Sanchez wake, MO anamkosa Mtu kama Said wa GSM pale Yanga, anamkosa Mtu kama Marina wa Roman Abramovich pale Chelsea ama Sheikh Tamim El Thani na Nasser El Khereffi pale PSG, huyu Tajiri wa Simba anaishi kwa upweke sana.

Ukimtazama Tajiri MO ni kama yupo kwenye msitu mzito sana, ambapo licha ya kutoa hewa safi, matunda na uoto mzuri wa asili ila bado Wanyama hawatoki kutoa sifa na wanakata sana miti yenyewe, anakosa mtu kama Jose Angel wa Real Madrid ambaye aliwahi kukunjana na Mjumbe wa bodi Manuel Redondo kisa kumsema vibaya Perez.

Tajiri Mpweke zaidi kwenye historia ya mpira ambaye alianza kuamini kwenye uwekezaji na kuweka pesa zake Msimbazi pasi na shaka, ila watu wakija nje hawasemi ukweli, Tajiri Mpweke zaidi kwenye historia ya mpira ameweka Billion 20 Benki na Simba inapokea mzigo wa Million 200 kila mwezi ila watu wamejificha hawasemi.

Tajiri Mpweke ana thamani sana wakati huu wa usajili anamwaga pesa ila mambo yakishaanza kwenda tofauti tutasikia simulizi za hatoi pesa, ameisusa timu! Mpaka pale Katiba itakaporuhusu Wanachama wapya kudahili basi Tajiri hatokuwa Mpweke tena.

By Farhan Kihamu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.