Kipa Djigui Diarra Atingisha Kiberiti Yanga...Kipa Djigui Diarra Atingisha Kiberiti Yanga...

KIPA wa Yanga, Djigui Diarra ametingisha kiberiti klabuni hapo kwa kuwataka viongozi wa kikosi hicho kumwongezea mshahara zaidi ili aendelee kusalia katika timu hiyo.

Taarifa zilizopo zinadai kipa huyo kutoka Mali, aliyejiunga na Yanga Agosti 8, 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao, amewaambia mabosi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu kwa misimu mitatu mfululizo thamani yake kwa sasa imepanda zaidi tofauti na mwanzo jambo linalomfanya kutaka kuboreshewa masilahi.

Kipa huyo ambaye mkataba wake alioongeza mwaka jana unafika mwishoni Januari 2025 na amekuwa ndiye nguzo ya Yanga katika kubeba mataji kwa misimu mitatu mfululizo na kuifikisha timu hiyo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.