Wajumbe wote wa bodi ya wakurugenzi wa Klabu ya Simba upande wa Mwekezaji Mohamed Dewji wamejiuzulu nafasi zao baada ya Mwekezaji MO kuwapigia simu akiwataka waandike barua za kujiuzulu kwa lengo la kuunda safu mpya ya uongozi kabla ya kuanza mchakato wa usajili mpya.
Wajumbe hao wa Bodi ni Mwenyekiti, Salum Abdallah 'Try Again', Dk. Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.
Kama mambo yataenda kama ilivyopangwa basi kuanzia muda huu Mwanadada Barbara Gonzalez atatangazwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa muda wa timu hiyo.