Suala la Kipa Ayoub Kubakia Simba au Kuondoka, Mchakato Mzima Upo Hivi

 

Suala la Kipa Ayoub Kubakia Simba au Kuondoka, Mchakato Mzima Upo Hivi

MAMBO mazuri kati ya klabu ya Simba na kipa namba moja wa timu hiyo, Ayoub Lakred, baada ya kukubalia kusalia ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa mashindano kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Imeelezwa kuwa baada ya mazungumzo kwenda vizuri pande zote mbili kati ya Simba na kipa huyo atasaini mkataba wa mwaka mmoja kabla ya kuondoka kuelekea kwao kwenye mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi.

Mtoa habari amesema mambo yameenda sawa baada ya Ayoub kukubali kusalia ndani ya timu ya Simba kwa msimu ujao kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

“Kulikuwa na mazungumzo yameenda vizuri, Ayoub anasalia Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na atasaini kabla ya kuondoka kuelekea kwao kwenye mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi,” amesema mtoa habari huyo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amekiri kiwa kuna wachezaji wapo kwenye mazungumzo na wengine kuongeza mkataba kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo.

Amesema wachezaji ambao wanahitaji wataongezewa mkataba akiwemo Ayoub Lakred mambo yanaenda vizuri na pia baadhi ya nyota wengine ambao wapo kwenye mipango ya msimu ujao.

“Wachezaji ambao wanatakiwa kubaki wote wataongezewa mkataba kabla ya kwenda kwenye mapumziko baada ya hapo tutaangalia usajili kwa wachezaji wapya, msimu huu tutaleta watu wenye ubora,” amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.