Mayele Afunguka "Licha ya Chuki Mitandaoni, Nikiamua Kurudi Yanga Watanipokea"


Fiston Mayele
Fiston Mayele
Pamoja na kwamba kumekuwa na vita kubwa juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, bado naamini kwa asilimia 100% kwamba nikirudi Yanga mashabiki watanipokea.

Kitu ambacho nimejifunza Tanzania ni kwamba mashabiki wengi huwa wanajali maslahi yao na sio ya wachezaji.

Kucheza misimu miwili ndani ya yanga ilikuwa ni furaha sana kwao, ila ilipofika hatua ya mimi kuondoka, watu walianza kunichukia bila sababu yoyote.

Mbona wachezaji wengi tuu wanaenda pale na kuondoka ila mimi tuu ndo wawe na chuki kubwa na mimi!!?, kosa langu kubwa liko wapi?..................

Japo kuwa naamini kabisa nikirudi napokelewa kwa sababu narudisha maslahi kwenye upande wa timu na mashabiki, ila sidhani kama wanachokifanya ni sahihi"

Mshambuliaji wa zamani wa @yangasc Fiston Mayele

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.