WAKATI ONANA AKIPIGWA BEI ….KITASA CHA ASEC MIMOSAS KUMRITHI INONGA SIMBA…

WAKATI ONANA AKIPIGWA BEI ….KITASA CHA ASEC MIMOSAS KUMRITHI INONGA SIMBA…

Winga wa Simba SC, Willy Esomba Onana ataondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huku SuperSport united wakiwa tayari wameonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Taarifa zinasema kuwa Simba sc wanataka kiasi Cha $75k ambayo ni sawa na milioni (194,550,976.00) za kitanzania ili kumruhusu aondoke ndani ya klabu ya Simba SC.

Willy Onana yuko tayari kuondoka klabuni hapo, klabu itatoa taarifa rasmi mara tu makubaliano yatakapofikiwa na Super Sports United ya nchini Afrika Kusini.


Katika hatua nyingine, Mlinzi wa ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra anatajwa huku Msimbazi kwenda kuziba pengo la Henock Inonga Baka ambae Taarifa zinaeleza kuwa mwishoni mwa msimu anaelekea AS FAR Rabat ya Morocco.

Nyota huyo raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 25 ameiongoza ASEC kutinga hatua ya robo Fainali ya CAF Champions League msimu huu akicheza michezo yote 12 ya ambayo ASEC Mimosas wamecheza kwenye michuano hiyo.

Inaelezwa kuwa Anthony Tra Bi anataka kuondoka ndani ya ASEC mwishoni mwa msimu huu na anataka kwenda kutafuta changamoto baada ya kuitumikia timu hiyo toka mwaka 2021. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.