Simba wapo kamili kwa Fainali Kombe la Muungano dhidi ya Azam

Simba wapo kamili  kwa Fainali Kombe la Muungano dhidi ya Azam

Benchi la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa lipo tayari kwa mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Aprili 27 2024 Uwanja wa New Amaan Complex.

Simba imetinga hatua ya fainali ya Muungano kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ inatarajiwa kukutana na Azam FC ambayo ilipata ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya KMKM.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa na wapinzani wao Azam FC sio timu ya kubeza lakini wapo tayari kwa mchezo huo.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Azam FC tunatambua kwamba Azam FC ni timu ngumu lakini maandalizi ambayo tumeyafanya yanatpa imani kwamba tunakwenda kufanya vizuri.

“Hii ni fainali hivyo haitakuwa nyepesi kikubwa ni utayari na tuna amini utakuwa ni mchezo mgumu hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Kocha Mkuu wa Azam Bruno Ferry ameweka wazi kuwa wanafuraha kwa kuwa wametinga fainali wanaamini watafanya vizuri kwenye mchezo wa fainali.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad