Msala Mpya Sakata la Kipa Kakolanya Kutoroka Kambini

Msala Mpya Sakata la Kipa Kakolanya Kutoroka KambiniUONGOZI wa Singida Fountaine Gate, umeendelea kusisitiza kuwa nahodha wao Beno Kakolanya ni mtoro kambini, huku pia wameweka wazi kuwa wanafanya uchunguzi kwenye suala la upangaji wa matokeo.
.
“Alichofanya ni utovu wa nidhamu, hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake, lakini pia kuna tuhuma zinafanyiwa kazi na kamati yetu ya nidhamu inafanyia kazi madai ya uhujumu katika mechi yetu dhidi ya Yanga, kamati ikikamilisha ripoti yake tutawafahamisha,” amesema Ofisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Masanza.
.
ARENA tulipomtafuta mchezaji huyo kuzungumzia sakata hilo alikataa kuongea chochote. Kakolanya alitoroka kambini muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu kati ya wageni, Yanga na wenyeji wa mchezo huo, Singida Fountain Gate.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.