Mayele "Nilivyotoka Yanga Yalinikuta Mazito, Bila Mwamposa Ningekufa"

Mayele "Nilivyotoka Yanga Yalinikuta Mazito, Bila Mwamposa Ningekufa"


Mchezaji wa Zamani wa Yanga na Sasa Pyramids Fiston Mayele ameeleza kuwa alipitia hali ngumu sana Kimwili na Kisaikolojia, kwani kabla ya kwenda kusaini mkataba katika klabu ya Pyramids ya Misri Mguu wake ulianza kuvimba na kumuuma mno.


Mayele ambaye ni raia wa Congo DR, amefunguka hayo wakati akifanyiwa mahojiano maalum na katika kipindi cha Wednesday Night cha Azam TV.


Mayele amesema baada ya kupatwa na tatizo hilo kawa anatembelea magongo, analala sebuleni kwani alikuwa hawezi kupanda ngazi za chumbani kwake, anaongeshwa na kufanyiwa kila kitu na mkewe, na mguu ulikuwa hatarini kukatwa kama ungeoza, hali hii ilimfanya kuona kuwa hataweza kucheza mpira tena katika maisha yake akawa akawa analia usiku na mchana.


Muda huo Pryamids walikuwa wakimuita aende kusaini mkataba hali iliyomfanya kuwadanganya kuwa amefiwa ili avute muda hadi apate nafuu, ikambidi aende kwao Congo ndipo akapata nafuu akaenda kusaini mkataba na siku tatu mbele Pyramids walipo-post picha yake kwenye mtandao wao ya kijamii, mguu ukavimba tena na kuanza kumuuma mno.


Mayele amesema alirudi Tanzania na kwenda kuombewa kwa Mchungaji Boniphace Mwamposa na akapata nafuu, na sasa anacheza hivyohivyo huku mguu ukiwa umevimba lakini kwa sasa hauna maumivu, huku akisisitiza kuwa mwisho wa msimu huu ataogea kila kitu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.