Julio: Yanga Wangeongeza Kasi Kidogo, Simba Tungepigwa Nyingi

Julio: Yanga Wangeongeza Kasi Kidogo, Simba Tungepigwa Nyingi


Kocha wa Singida Fountain Gate FC na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa wachezaji wa Simba ni kama wamechoka na wanashindwa kujituma uwanjani na kusababisha timu hiyo kukosa matokeo.


Julio amesema kuwa iwapo kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Yanga, wapinzani wao hao wangeongeza jitohada kidogo basi Simba angefungwa bao nyingi zaidi ya zile 2-1 waliofungwa kwenye mchezo huo.


“Hata huko nyuma ilishawahi kutokea Simba alishafungwa na yanga namna hii n ahata Yanga alishafungwa na Simba kwa namna hii. Mechi ya kwanza Simba walifungwa bao tano, kuna makosa yalifanyika, mechi hii kilichowashusha ni morali ya wachezaji wa Simba kuwa chini lakini pia kujiamini kwa wachezaji wa Yanga imewaonesha kuwa wanataka kushinda.


“Kutoana na matokeo mabovu ya hivi karibuni, morali ya wachezaji wa Simba ilikuwa juu na wanacheza kama wamelazimishwa, hawakuwepo uwanjani na kama Yanga wangeongeza kasi kidogo kama mechi iliyopita, sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine zaidi.


“Tatizo liko kwa wachezaji sababu kocha anafanya sehemu yake na anawaachia wachezaji sehemu yao, leo Benchikha utamlaumu kwenye kitu gani? Angali Yanga, kujituma ndicho kimewapa matokeo, wanakaba sana, wakipata mpira wanataka kutuadhibu haraka, second balls wanawahi wao, kila wanachokifanya wako sahihi, Simba ni kama tulikuwa tunacheza bonaza, watu wanajivuta, kama kuna kitu waseme.


“Wachezaji wanatakiwa wafanyiwe ushauri kuwajenga kisaikolojia ili kumsaidia mwalimu kwa kutumia malejendi. Wapo watu wengi ambao wameitumikia Simba wanaweza kupata nafasi ya kwenda kuzungumza na wachezaji. Yanga wanawajali wachezaji wao wakongwe, wanapewa basi wanakuja uwanjani ila sio Simba.


“Zamani Simba tulikuwa tukiwa na matatizo tunafungwa, lakini Yanga wakiwa na matatizo, wachezaji wao wakati ule huwafungi hata kama kuna ugomvi wa klabu,” amesema Julio.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.