GAMONDI AWAANDALIA KIPIGO KIZITO COASTAL UNION

 

GAMONDI AWAANDALIA KIPIGO KIZITO COASTAL UNION

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amesema kuelekea mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Coastal Union, amejiandaa kukutana na mpinzani mgumu, hivyo tayari ana mbinu za kushinda.

Kesho Jumamosi, timu ya Young Africans SC itakuwa mwenyeji wa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 12:00 jioni.

“Kesho mchezo utakuwa mgumu, tutapambana kadiri ya uwezo wetu. Tuna hasira, kwetu huu ni mchezo muhimu, tunafahamu tunakwenda kucheza dhidi ya timu ngumu, inazuia vizuri, tutaona kesho ambapo tutajitahidi kufanya vizuri kukaa zaidi kileleni.

“Kimbinu hatujajiandaa sana, jana tulikuwa na mazoezi ya kujiweka sawa, leo tutakuwa na mazoezi kidogo, hatuhitaji kujiandaa sana kimbinu, tunafahamu tumeshacheza mechi zaidi ya 40 msimu huu katika michuano yote, hivyo kwa sasa ni kuangalia namna ya ubora wa wachezaji uamue mchezo.

“Kesho angalau tunakwenda kucheza katika uwanja ambao tutacheza vizuri, sio kama ule uliopita ambao ni hatari kuchezea, ubora wa wachezaji na mbinu zitaonekana.

“Sisi tunahitaji pointi kuendelea kukaa zaidi kileleni, Coastal Union wanahitaji pointi kudhihirisha kiwango walichonacho msimu huu, ninaamini utakuwa mchezo mzuri.

“Tunatarajia kukutana na mchezo wa tofauti hasa katika ulinzi, tunapaswa kujipa nafasi, kujaribu kupenya, kupiga mashuti na kutengeneza nafasi za kufunga ili kuwa na mchezo bora mbele ya mpinzani,” alisema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.