Fiston Mayele "Wakati Nasign Yanga Nilikuwa Sijui Kingereza, Mkataba Wangu Ulikuwa Mbovu"


Fiston Mayele "Wakati Nasign Yanga Nilikuwa Sijui Kingereza, Mkataba Wangu Ulikuwa Mbovu"

“Mkataba wangu wa kwanza Yanga haukuwa mzuri nilikuwa hata siwezi kuondoka, nilikuwa sijui kingereza, meneja wangu nae hajui kingereza anacheka cheka tu na viongozi, mkataba ulikuwa mgumu, mimi nimesaini tu nicheze nionekane.

“Baada ya kucheza msimu wa kwanza kuna timu ilikuja inanitaka nikawaambia mimi siondoki natakiwa kucheza msimu wa pili, wakaniambia utaongeza mkataba mwingine, nikawaambia sawa lakini nakuja na meneja mpya sio yule wa kucheka cheka hovyo.

“Nikampa mkataba Yasmin akashtuka akanisaidia tukabadilisha mkataba ndio nikasaini mkataba mpya hata Pyramids nimekuja kusaini naye,” Fiston Mayele akizungumza na Azam Media.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.