EDO Kumwembe "Fiston Mayele Anaumia Sana Kuona Yanga inafanikiwa Bila yeye"

 

EDO Kumwembe "Fiston Mayele Anaumia Sana Kuona Yanga inafanikiwa Bila yeye"

 EDO Kumwembe "Fiston Mayele Anaumia Sana Kuona Yanga inafanikiwa Bila yeye"

Kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya soka, Edo Kumwembe ambaye amefunguka sakata la mshambuliajiwa Pyramids Fc ya Misri, Fiston Mayele kuwatupia madongo waajiri wake wa zamani, Klabu ya Yanga.


“Nadhani kuna tabia ambayo Mayele aliificha akiwa Young Africans na sasa ameifichua. Kutaka kuonekana mkubwa na mfalme. Bahati mbaya inamuumiza pia kwamba Young Africans wanasonga mbele bila ya yeye. Huwa inatokea unapoachana na mpenzi wako. Hautaki yamtokee mema mbele ya safari.


Lakini kuna uwezekano mkubwa Mayele anaumwa ugonjwa wa kupenda nyumbani (home sickness). Tayari Tanzania kulishakuwa nyumbani kwake na aina ya maisha ya Tanzania yalimuingia kwelikweli. Maisha ya uwanjani, mitaani na mitandaoni. Tanzania bado haijamtoka. Bado ipo akilini mwake. Mwili upo Misri, lakini akili ipo Tanzania.


Inawatokea wageni wengi waliowahi kuishi Tanzania. Sio tu wanasoka kama kina Bernard Morrison ambao tunaona kila siku wanazurura Dar es salaam ingawa wanacheza soka la kulipwa Morocco, lakini pia kwa wageni wengine. Hata kuna mabalozi wa nchi za nje hawaishi kurudi kutembea Tanzania baada ya muda wao kuisha," amesema Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.