BILIONI 19.2 KUKARABATI UWANJA WA UHURU

 

BILIONI 19.2 KUKARABATI UWANJA WA UHURU

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini Mkataba wa ukarabati wa uwanja wa uhuru uliopo jijini Dar es salaam na kampuni ya CRSEG ya China.

Katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo Serikali imeweka wazi gharama itakayotumika kukarabati huo ni bilioni 19.2 za Kitanzania na ukarabati huo utachukua miezi 12 sawa na mwaka mmoja.

Hongera Serikali kwa hatua hii ambayo inatoa mwanga kuelekea michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ ambayo Tanzania, Kenya na Uganda watakuwa wenyeji kwa pamoja.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.