Benchikha ni Kocha Mzuri Lakini Ana Bahati Mbaya - Mchambuzi

Benchikha ni Kocha Mzuri Lakini Ana Bahati Mbaya - Mchambuzi


Mchambuzi wa michezo Farhan Kihamu anasema Kocha, Abdelihak Benchikha ni kocha mzuri sema amekosa bahati tu.


Farhan amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa watani zao Yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi Aprili 20, katika Dimba la Mkapa.


"Ukitazama mechi dhidi ya Yanga utakubaliana na Mimi kuwa huyu Benchika ni Kocha mzuri sana ambaye kwa bahati mbaya sana ana kikosi cha Wachezaji wengi wa kawaida sana.


"Ni Kocha mshindi ambaye ameshinda mataji mengi akiwa na vikosi bora sana, bahati mbaya sana yupo kwenye timu yenye kikosi cha kawaida sana, ndio maana ana wachezaji wake 13 tu wa maana ambao anawatumia.


"Kama ataendelea kusalia ni kudidimiza CV yake kwa kuendelea kukaa na kundi la Wachezaji wengi wa kawaida, mpatieni Mkurugenzi wa Ufundi, wakae na Scouts waunde project mpya ambayo inataka PESA, PESA, PESA, apewe pesa alete Wachezaji wa daraja lake ili afanye nao kazi."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.