Wenyeji Yanga SC wametoa sare ya bila kufungana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jana usiku Uwanja wa BenjamÃn Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Licha ya kucheza bila nyota wake watatu wa kikosi cha kwanza ambao wote ni majeruhi, beki Kouassi Attohoula Yao, viungo Peadoh Pacome Zouazoua wote Waivory Coast na Mganda Khalid Aucho, lakini Yanga ilifanikiwa kuimudu Mamelodi, klabu bora kwa sasa Afrika kwa mchezo wa kujihami zaidi.
Angalau kipindi cha pili Yanga walianza kumiliki mpira, lakini muda mrefu walibaki kwenye eneo lao na kushambulia kwa kushitukiza.
Timu hizo zitarudiana Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katà ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.