Simba Waanza Mazungumzo na Singida Fountain Gate Kumsajili Kibabage Kutoka Yanga


Nickson Kibabage
Nickson Kibabage

Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Simba imeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Singida Fountain Gate, Nickson Kibabage ambaye yupo Yanga Sc kwa mkopo.

Imeelezwa kuwa tayari Simba wameanza kufanya mazungumzo na Singida juu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Singida utafikia ukomo mwaka 2025.

Kibabage yupo Yanga kwa mkopo wa miezi sita baada ya mkopo wa awali ulioanza Julai 2023 kufikia tamati na Yanga kuamua kuongeza mkataba mwingine alioanza kuutumikia Januari 2024 na utafikia tamati Juni 2024.

Ikumbukwe kuwa Kibabage alitua Singida FG akitokea Mtibwa Sugar ambapo Singida iligharamika zaidi ya milioni 100 kuinasa saini ya beki huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.