Mayele kurejea Yanga? |
Meneja wa Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Pyramids ya Misri, Fiston Kalala Mayele aliyemleta Tanzania Nestor Mutuale, amesema kuwa mchezaji huyo bado anaiheshimu Yanga SC ambayo imemuweka kwenye ramani ya soka la ushindani Kimataifa.
Kauli hiyo ya Mutuale inakuja baada ya vyombo vya habari nchini Tanzania kuripoti kuwa mshambuliaji huyo aliyefanya makubwa kwa misimu miwili mfulululizo na Wananchi wa Jangwanai anataka kuhamia kwa wapinzani wao Simba SC baada ya kushindwa kufanya vizuri nchini Misri.
"Mteja wangu anajua vizuri thamani na jukwaa ambalo Young Africans walimpatia kama itabidi kurudi Tanzania basi nafasi ya kwanza watapewa Young Africans Ila kwa sasa ana furaha ndani ya Pyramid labda mengine yatokee mbele lakini kwa sasa yuko na furaha," amesema meneja wa Mayele.
Yanga wanatajwa kufikia makubaliano mazuri na aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube baada ya kutemana na matajiri hao wa Dar es Salaam.