Hassan Dalali: Niliuza friji langu kulipa Mishahara ya Wachezaji Simba

Hassan Dalali: Niliuza friji langu kulipa Mishahara ya Wachezaji Simba


Mwenyekiti mstaafu wa Simba Hassan Dalali, ametukumbusha mkasa wake wa kuuza friji ili tu aweze kuwalipa mishahara wachezaji wa Simba wakati akiwa kiongozi wa timu hiyo.


Amesema kipindi cha nyuma klabu hiyo ilipitia ukata mkubwa wa kifedha, kiasi cha kupelekea kushindwa kumudu kulipa mishahara ya wachezaji tofauti na sasa wakati huu wa uwekezaji.


Amefunguka hayo alipozungumza na kipindi cha michezo cha The Scoreboard hapa Times Fm.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.