Timu ya SIMBA Kifua Mbele Wapania Kuua Mtu, Watua Botswana Kifalme |
Wekundu wa Msimbazi Simba SC tayari wamewasiri nchini Botswana tayari kwa ajili ya kupepetana na Jwaneng Galaxy hapo kesho Desemba 2, 2023.
Simba wamewasiri wakiwa na wachezaji 20 pamoja benchi zima la ufundi linaoongozwa na Benchikha.
Simba itacheza mchezo huo ambao utakuwa wa pili wa Makundi ya Klabu Bingwa Afrika mara baada ya mchezo wa awali kutoka sare ya 1-1 dhidi ya ASEC Mimosas katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
Jwaneng wao mchezo wa awali walikuwa ugenini dhidi ya Wydad Casablanca na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0.
mungu awape wepesi tupate pointi 3 mihi
ReplyDelete