Kisa Yanga Kusua sua Ligi ya Mabingwa Max Nzengeli Kaibuka na Hili Tena

Kisa Yanga Kusua sua Ligi ya Mabingwa Max Nzengeli Kaibuka na Hili Tena


Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo na Klabu ya Young Africans Maxi Mpia Nzengeli amesema kuwa licha ya kutokupata ushindi katika michezo iliyopita ya Ligi ya Mabingwa, bado wanayo nafasi ya kushinda michezo ijayo na kufuzu kwenda katika hatua inayofauata ya michuano hiyo.

Maxi Nzengeli katika michezo yote ya makundi ambayo ameichezea Young Africans ameshindwa kufunga bao lolote tofauti na kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo amefanikiwa kuifungia Young Africans mabao saba.

Maxi amesema kuwa michezo ijayo ambayo imesalia wataitumia vyema katika kuhakikisha kuwa wanapambania kupata ushindi ili waweze kuvuka hatua hii ya makundi na kwenda katika hatua ambayo inafuata ya michuano hiyo.

“Ndio haijawa nzuri kwetu, kushindwa kupata ushindi katika mchezo wowote kati ya michezo mitatu ambayo imepita, hilo jambo linatuumiza kama wachezaji, jambo lingine ni kuwa katika nafasi ya mwisho kwenye kundi letu hili pia linatuuumiza haswa.

“Kikubwa kwa sasa ni kutokukata tamaa kwani naamini kuwa bado tunayo nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa tunafanya vyema katika michezo ijayo, kushinda katika kila mchezo, naamini nafasi ya kufuzu bado ipo kwa kuwa tunaona ugumu wa kundi letu lakini nikuhakikishie kuwa hatujakata tamaa sisi kama wachezaji,” amesema Maxi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.