Bocco, Aishi waachwa Dar Simba ikielekea Botswana

 

Bocco, Aishi waachwa Dar Simba ikielekea Botswana

Nyota wa Simba Kapteni John Raphael Bocco na golikipa Aishi Manula, wawapo kwenye orodha ya wachezaji waliokwea pipa alfajiri ya leo Desemba , 2023 kuelekea nchini Botswana kuwakabili Jwaneng Galaxy.

Kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchika, wapo wachezaji wote tegemeo isipokuwa Bocco na Aishi na Wekundu hao wa Msimbazi hawajatoa taarifa za kuachwa kwa wachezaji hao licha ya kufanya mazoezi na timu siku chache kabla ya safari.


Orodha kamili ya wachezaji waliosafiri ni hii hapa:


Magolikipa: Ayoub Lakred, Ally Salim na Hussein Abel.


Mabeki: Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Fondo Malone, Henock Inonga, Kennedy Juma, Israel Mwenda na Hussein Kazi.


Viungo: Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Saidi Ntibanzonkiza, Luis Miquissone na Willy Essomba Onana.


Washambuliaji: Jean Baleke, Moses Phiri na Kibu Denis

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.