Yanga Vs Al Ahly |
Mchambuzi wa soka Bongo Master Tindwa amesema, Al Ahly waliwazidi Yanga SC kwa ubora na ndio maana kulikuwa na utofauti mkubwa kwenye mechi hiyo ya Klabu Bingwa iliyochezwa jana Desemba 2, 2023.
Alisema Al Ahly wachezaji wao ni bora kulilo wa Yanga.
“Al Ahly wana quality ya mchezaji mmoja mmoja, tunaposema Yanga ina wachezaji wenye quality unawalinganisha na nani?"
“Mbinu za mwalimu Gamondi ukilinganisha na Al Ahly ni tofauti kabisa ,kipindi cha pili Al Ahly wametawala mchezo kiasi kwamba unajiuliza Yanga watapata goli ? Na kama watapata atafunga nani ? Bahati nzuri wamepata goli lakini ni la uwezo binafsi”alisema Master Tindwa kuhusu Yanga ambao wanashika mkia kwenye kundi lao wakiwa na alama moja kwenye mechi mbili hadi sasa