Ahmed Ally Anachonganisha Mashabiki wa SIMBA na Uongozi

 
Ahmed Ally Anachonganisha Mashabiki wa SIMBA na Uongozi
Ahmed Ally

Ahmed Ally Anachonganisha Mashabiki wa SIMBA na Uongozi

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Timu hiyo, Ahmed Ally amekuwa akitoa kauli ambazo ni kama zinachonganisha kati ya viongozi na mashabiki pamoja na wachezaji wa timu hiyo.

Mchombe amesema hayo kufuatia Ahmed kuwahamisha mashabiki wa Simba kwenda uwanjani kuishuhudia timu hiyo kwamba ingefanya vizuri lakini mwisho wa siku inafanya vibaya na kushindwa upata matokeo chanya.

“Tatizo la msemaji wa Klabu (Ahmed Ally) ni mchonganishi, anatuchonganisha mashabiki, wachezaji na uongozi. Ukimsikiliza Ahmed unapokuja uwanjani unasema leo tunaua mtu bao 4.

“Mechi ya ASEC alisema tunajua mashabiki mmeumia na sisi tumeumia, njoo na maumivu yako, utarudi na furaha. Shabiki anakuja uwanjani akiamini timu yangu inakwendsa kushinda, timu ikipata suluhu lazima watu wachukie.

“Ila kilichonikera ni mashabiki kusubiri kuzomea wachezaji baada ya mechi, huo ni ushamba waachane na haya mambo, Simba hatuko huko, tafuta media toa maoni yaoko viongozi watayapata.

“Tunatakiwa tuje uwanjani na kuishabikia timu irudi kwenye msitari lakini tukikata tamaa, Simba inakufa,” amesema Mchome.


SOMA PIA: Ligi Bora Africa | Best Football Leagues in Africa 2023/2024


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.