Yanga Yapigwa Faini Milioni 5, Simba Faini Milioni 1

Yanga Yapigwa Faini Milioni 5, Simba Faini Milioni 1

Yanga Yapigwa Faini Milioni 5, Simba Faini Milioni 1

Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu Soka Tanzania imevitoza faini Vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanya makosa kadhaa katika mchezo dhidi yao uliyochezwa Novemba 5 2023 na Yanga kushinda 5-1.

Kamati hiyo imeipiga Yanga faini ya Tsh. milioni 5 kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango sio rasmi kuelekea mchezo huo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Klabu ya Simba SC imetozwa faini ya Tsh. milioni 1 kwa kosa la Wachezaji wake kuchelewa kutoka vyumbani na kupelekea mchezo huo kuchelewa kuanza kwa takribani dakika 4 kutoka vyumba vya kubadilishia nguo na kupelekea kuharibu program za mrushaji matangazo (Azam TV).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.