Walichokifanya Yanga ni Ushamba Mkubwa - Mchambuzi

 

Walichokifanya Yanga ni Ushamba Mkubwa - Mchambuzi

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Ahmad Mkunda amesema kuwa kitendo cha Klabu ya Yanga kuweka bango barabarani kuwazodoa wapinzani wao Simba Sc ni ushamba ambao umepitwa na wakati.

Mkunda amesema hayo baada ya Yanga kuweka bango barabarani linaloonyesha mabao 5-1 waliyowafunga wapinzani wao Simba, Novemba 5, 2023.

"Wanachokifanya Yanga kulipia gharama ya kuweka mabango barabani baada wakinadi ushindi wao wa 5-1 dhidi ya Simba huu ni ushamba. Ni bora waweke nguvu zaidi kujiandaa na Michezo Yao ya Hatua ya makundi ya Klabu Bingwa," amesema Mkunda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.